Friday, December 14, 2012

JINSI YA KUTENGENEZA VEGETARIAN PIZZA


 

Mahitaji

1) 3 kikombe cha chai au (400g).

2) 2 tsp vya amira.

3) 2 tsp vya chumvi

4) 1 kikombe cha chai maji ya moto

3) 3 tsp ya mafuta (pendekezo olive oil)

4)Piilipili hoho kubwa 1

5)1 tsp tangawizi yakuponda

6)1 tsp ya kitungu swaumu kuponda

7)1/4 tsp ya binzari tamu

6)3/4 nyanya tunda

7)1/4 nyanya ya kopo

8)1/2 pili

9)1/2 tsp pilimanga

10)1/2 cheese/butter

11)1kitungu maji kikubwa

 

Baada kuwa na mahitaji hayo changanya unga ,amira na chumvi ukishachanganya weka maji  yako ukande kwa dakika 7-10.Ukimaliza weka dida kwenye bakuli  funika na kitamba kisafi acha kama dakika 30.Kisha kandakanda tena kwa sekunde chache ,baada yahapo chukua dida linyooshe liwe katika ubo la duara weka kwenye sahani .

Chukuwa dida lako paka butter kwenye didia vizuri pande zote.baada ya hapo weka  mafuta ya kwenye chombo cha kukangia ya pate moto alafu mimina kitungu ,vitungu vikiwa vya brouwn weka kitungu swaum na tangawizi baada ya hapo weka pilipilihoho ulilokatakata kwa dakika5 (sema uwe mwangalifu hoho lisibadilike rangi yake),weka nyanya tunda ulilokatakata na koraga kwa dakika 2-3 baada ya hapo weka binzari tamu koroga,weka chumvi,pilipili,pilipili manga koroga kwadakika2 baada ya changanyiko wetu kuwamzito weka nyanya ya kopo,koroga kwa  dakika 5.baada ya hapo itakuwakama hiyo

 

Ok! baada ya hapo kama mnavyoona vegitable souce yetu iko tayari,kinachofwata nikuimiminizia kwenye lile dida  letu vizuri bila ya kuacha nafasi iliokosa vigetable alafu weka cheese yako ambayo ulisaga mikato midogodogo miminizia kwa juu pande zote.

Baada yahapo iweke kwenye oven moto uwe normal kama dakika 5 mpaka ile cheese yetu inayeyuka na pizza kuiva.

 

PIZZA IKO TAYARI KWA KULIWA

 

 

 Unaweza ukaila kwa wine au juice yeyote uipendayo.

0 comments:

Post a Comment