Friday, December 14, 2012

MAPISHI YA NGURU WA NAZI NA BAMIA
MAHITAJI
Samaki nguru   5 vipande

Thomu na Tangawizi iliyosagwa   1 kijiko cha supu

Pilipili mbichi iliyosagawa  kijiko cha supu

Pilipili nyekundu ya unga  1 kijiko cha chai

Bizari ya mchuzi 1  kijiko cha chai

Ndimu 2 kamua maji

Chumvi kiasi 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika Nguru

 Changanya vitu vyote katika kibakuli ufanye masala ya kupaka kwenye samaki.
Roweka kwa muda nusu saa
Paka treya mafuta, kisha mpange nguru na mchome katika oveni.
Atakapoiva upande upande mmoja mgeuze upande wa pili huku unanyunyizia mafuta.
 Epua weka kando.

 

Vipimo vya mchuzi

Vitungu maji
Nyanya 2

Tuwi zito la nazi  2 vikombe viwili

Bamia 1 kikombe

bizari ya manjano  ¼ kijiko cha chai

Pilipili mbichi 1

Ndimu  na chumvi kiasi

 NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
Katika sufuria tia tuwi kikombe kimoja, kisha tia bamia ulizokatakata zipike ziwive kidogo.
Saga kitunguu, nyanya na pilipili mbichi katika mashine ya kusagia (blender) kisha mimina katika tui la bamia.
Tia vipande vya nguru, bizari, chumvi, ndimu, kisha tia tui lilobakia.
  Acha mchuzi uchemke kidogo kidogo kisha epua utie katika bakuli ukiwa tayari.
(by alhidaya)

MAPISHI YA  BISKUTI ZA JAM

MAHITAJI 
1. Unga wa Ngano 2 vikombe
2.Olive oil Sukari  
3.Sukari robo                                     
4. Baking powder 2 tsp
5.Mayai 2
6.Flovour yeyote(strawberry,vanilla ,choclate n.k)1tsp
 
NAMNA YA KUTAYARISHA 
 
  • Changanya sukari ,mayai,flavour yako na olive oil koroga ikiwezekana isage kwenye blenda. Tia unga kwenye bakuli pamoja na baking powder, mimina vitu ulivyosaga kwenye bakuli, changanya.
  • Punguza unga uliochanganya kidogo weka pembeni.--  Unga uliobakia tia kwenya tray ya kuchomeya, utandaze vizuri, tia jam juu yake.
  • Chukua la kukwaruzia carrot (grater) ukwaruze unga uliuopunguza juu ya jam.
  •  Choma kwa muda dakika 20 moto wa 180 C. 
  • Acha ipowe kidogo, zikate vipande vya mraba (square) Tayari kwa kula.


 
 

JINSI YA KUTENGENEZA VEGETARIAN PIZZA


 

Mahitaji

1) 3 kikombe cha chai au (400g).

2) 2 tsp vya amira.

3) 2 tsp vya chumvi

4) 1 kikombe cha chai maji ya moto

3) 3 tsp ya mafuta (pendekezo olive oil)

4)Piilipili hoho kubwa 1

5)1 tsp tangawizi yakuponda

6)1 tsp ya kitungu swaumu kuponda

7)1/4 tsp ya binzari tamu

6)3/4 nyanya tunda

7)1/4 nyanya ya kopo

8)1/2 pili

9)1/2 tsp pilimanga

10)1/2 cheese/butter

11)1kitungu maji kikubwa

 

Baada kuwa na mahitaji hayo changanya unga ,amira na chumvi ukishachanganya weka maji  yako ukande kwa dakika 7-10.Ukimaliza weka dida kwenye bakuli  funika na kitamba kisafi acha kama dakika 30.Kisha kandakanda tena kwa sekunde chache ,baada yahapo chukua dida linyooshe liwe katika ubo la duara weka kwenye sahani .

Chukuwa dida lako paka butter kwenye didia vizuri pande zote.baada ya hapo weka  mafuta ya kwenye chombo cha kukangia ya pate moto alafu mimina kitungu ,vitungu vikiwa vya brouwn weka kitungu swaum na tangawizi baada ya hapo weka pilipilihoho ulilokatakata kwa dakika5 (sema uwe mwangalifu hoho lisibadilike rangi yake),weka nyanya tunda ulilokatakata na koraga kwa dakika 2-3 baada ya hapo weka binzari tamu koroga,weka chumvi,pilipili,pilipili manga koroga kwadakika2 baada ya changanyiko wetu kuwamzito weka nyanya ya kopo,koroga kwa  dakika 5.baada ya hapo itakuwakama hiyo

 

Ok! baada ya hapo kama mnavyoona vegitable souce yetu iko tayari,kinachofwata nikuimiminizia kwenye lile dida  letu vizuri bila ya kuacha nafasi iliokosa vigetable alafu weka cheese yako ambayo ulisaga mikato midogodogo miminizia kwa juu pande zote.

Baada yahapo iweke kwenye oven moto uwe normal kama dakika 5 mpaka ile cheese yetu inayeyuka na pizza kuiva.

 

PIZZA IKO TAYARI KWA KULIWA

 

 

 Unaweza ukaila kwa wine au juice yeyote uipendayo.